shuku image TIA MBEYA

Wednesday, May 16, 2012

Biashara ya kununua/kuuza nje ya nchi (import-export)

Wapendwa wasomaji nachukua fursa hii kuwashukuru kwa dhati wasomaji wote walionipa mrejesho (feedback) katika mada ya wiki iliyopita tulipogusia kidogo juu ya kupanua biashara nje ya nchi.
Zaidi ya wasomaji 245 wameomba mada hii niiweke kwa upana zaidi. Nami sina ajizi kwani inanipa moyo kuwa kuna wajasiriamali wengi wanalenga kupanua biashara zao nje ya mipaka ya Tanzania ambapo itawaingizia faida zaidi na hata kwa upande wa nchi itaongeza pato la taifa (GDP) na kuinua uwiano wa bidhaa zinazoletwa nchini na zile zinazouzwa nje ya nchi (balance of payment- katika dhana ya kawaida).
Hivyo basi kuweka mada hii katika mapana yake  tutakuwa na mfululizo (series) wa mada kwa wiki 5 itakayohusu mambo ya msingi katika biashara ya kununua/kuuza nje ya nchi, kutengeneza mahusiano kibiashara, mchanganuo wa soko, wapi utapata msaada, namna ya kukutana na jamii ya wajasiriamali wanaojihusisha na biashara za kimataifa, upatikanaji na uuzaji wa bidhaa, makubaliano ya kibiashara, kufanya mauzo, taratibu za kusafirisha bidhaa (terms of shipping), utumiaji wa mawakala wa usafirishaji (freight forwarder), barua ya udhamini ( letter of credit), upokeaji bidhaa, namna ya kutangaza bidhaa nje, kupanua biashara na kukuza/kustawisha biashara ya kununua/kuuza nje. Nakusihi usikose  kupata nakala ya gazeti lako pendwa kila wiki ili kupata mfululizo wa mada hii adhimu.
Ni njia gani za kuanzisha biashara yenye mafanikio na unayoweza kuipenda? Biashara ya kununua/kuuza (import/export) nje ya nchi inaweza kuwa jibu lako. Si kwamba inahitaji tu mtaji mdogo kuanza bali pia inakupa fursa ya kukutana na wateja mbalimbali ulimwenguni kote. Hauhitaji uzoefu mkubwa kufanya biashara hii, japo unahitaji uwezo mzuri wa kuratibu na kusimamia mambo. Kufanya biashara hii istawi kunahitaji taarifa na umakini wa mambo muhimu sana.
Je wewe unazalisha bidhaa na ungependa kupanua soko nje ya nchi? Au je una mpango wowote wa kusafiri nje ya nchi ili kupata taarifa kwa ajili ya kuanzisha biashara? Kama una uwezo wa kushawishi wateja na uwezo wa kufanya mahusiano ya kimataifa, biashara ya kununua/kuuza nje ya nchi inaweza kuwa nzuri kwako. Unachohitaji ni ari na malengo ya kufanikiwa.
Kadili utakavyoendelea kufanya biashara, utaelewa mambo mengi na namna ya kutatua changamoto. Mathalani unaweza kuhitaji mtu wa kusimamia masuala ya usafirishaji (freight forwarder). Na ungependa kuwa na mawasiliano na uhusiano mzuri na wagavi (suppliers). Lakini baada ya muda fulani unaweza kufanya mwenyewe taratibu hizo kwa gharama nafuu.
Faida nyingine ya kununua/kuuza nje ya nchi ni uzoefu wa kimataifa na faida halisi kutokana na biashara. Mara unapokuwa umezoea biashara, gharama ya kufanya mauzo inakuwa ndogo sana.
Na baada ya kuwa umejiimarisha na kuwa na wateja wa kutosha, utaona muda wako wote unaingiza pesa tu. Ichanganue biashara ya kununua/kuuza nje ya nchi, angalia vihatarishi (risks), na pima faida. Ongea na watu mbalimbali wafanyao biashara kama yako ili kujipima.

INAWEZEKANAJE
Kwa mujibu wa takwimu za Word Bank (Doing business in Tanzania - 2011) uzalishaji unaofanyika Tanzania ni 0.2% tu ndio inauzwa nje ya nchi. Kimsingi bidhaa ambazo huuzwa nje ni zile zitokanazo na kilimo na mapambo.
Ni dhahili kila mzalishaji wa bidhaa angependa kupanua soko lake hadi nje ya nchi, lakini si rahisi sana kwa kampuni au biashara yenye upeo na uwezo mdogo.
Si ajabu nawe msomaji ukawa katika kundi hili. Cha kufanya unaweza kutafuta mawakala nje ya nchi kwa ajili ya kusambaza bidhaa zako.
Changamoto iliyopo kwa wazalishaji wengi Tanzania hakuna ubunifu wa kutosha na ari ya kujituma kuzingatia ubora na viwango vya bidhaa wanazozalisha. Hivyo ni msingi kutafuta mawakala au watu wanaoweza kukupatia maelekezo mazuri ya vigezo na namna utakavyouza bidhaa zako nchi za nje.
NAMNA YA KUANZA  
Biashara hii ya kuuza/kununua nje pia unaweza kuanzia nyumbani kwako kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii mfano facebook, twiter, email, n.k. unachohitaji ni mfumo mzuri wa kutunza taarifa, kuwa na business card, kuwa na komputa pamoja na simu aidha ya mezani au ya mkononi inayopatikana endapo mteja atahitaji kuwasiliana kwa njia hii.
Baada ya biashara kusimama utahitaji kujiimarisha zaidi kimawasiliano. Pia utahitaji kuwa na nembo na anuani ya biashara (letter head), kibiashara nembo ndiyo inakuwakilisha hivyo ni muhimu sana iwekwe kitaalam. Itaendele…………..+255753686848

Zijue taratibu za kuanzisha biashara

na shukran mwakisu
Wapendwa wasomaji ni wiki nyingine tena kama ada tuanze kwa kumshukuru Mungu kutujalia uhai. Napenda kutumia fursa hii kuwashawishi baadhi ya watu wanaofikiria kuanzisha biashara.
Bila shaka endapo msomaji  anafanya biashara atakuwa   amepata mambo matatu ambayo yatakusaidia kurekebisha mahali ambako ulikosea.

Je, ni njia zipi unapaswa kupitia ili kuwa mjasiriamali? Hili ni swali  gumu sana kwa sababu majibu yanatofautiana.
Kama hujawahi kufikiria kuwa mjasiriamali na inatokea bahati mbaya unatafuta kazi, lakini hujapata na ukaamua kuanzisha biashara utakuwa katika wakati mgumu kupata mafanikio.

Lakini kwa mtu mwingine ambaye amekuwa akifikiria kuwa mjasiriamali, hakika ukianza biashara utakuwa katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.
Zifuatazo ni mbinu za kuwa mjasiriamali bora:
1. Elimu: Pata taarifa mbalimbali za ujasiriamali fahamu faida na changamoto. Pia fahamu tabia za wajasiriamali waliofanikiwa ujenge taswira ya mjasiriamali wa namna gani utakuwa. Mathalani kama bado uko shule au chuo hudhuria vipindi vingi vya elimu ya ujasiriamali.
Kama hauko shule, tafuta namna yoyote upate elimu mfano elimu ya watu wazima, makongamano, warsha, midahalo, mafunzo, kuangalia televisheni na sikiliza redio. Angalizo: jipangie muda maalumu ili usitumie muda mwingi kujifunza na kuchelewa kuanza biashara. Suala la elimu linaendelea hata baada ya kuanzisha biashara.
2. Jenga ndoto kubwa: Katika hatua nyingine ili kuwa mjasiriamali bora, weka mikakati ya kwamba unataka kuwa mjasiriamali wa aina gani. Fikiria miaka mitano, kumi mpaka 20 itakuaje. Pia fikiria namna gani utaiendesha biashara ya ndoto yako.
Katika hatua hii usisumbuke kufikiria namna ya kupata fedha ya kuanzisha biashara. Kama utaanza kuwa na wasiwasi wapi utapata fedha, pia hutaweza kuanza biashara.
Katika hatua hii, wasiliana na watu mbalimbali wenye biashara, waulize walianzaje. Pia fikiria mambo makubwa. Usiwaze kufanya vitu vidogo ambavyo kila mtu anaweza kufanya.
3. Mipango: Baada ya kujenga ndoto yako, andika mipango mbalimbali jinsi ya kuanzisha biashara. Mipango hii sio mchanganuo wa biashara bali andika mambo mbalimbali unayojifunza kutoka kwa wajasiriamali wenzako na tunza vizuri taarifa hizo.
Kama umenunua gazeti na kuona habari njema kwako chana kipande na tunza, inapendeza ukiwa na faili au hata bahasha fulani hivi tunza vipande vya karatasi unazoandika mambo yako siku moja utaifungua na utagundua una taarifa nyingi za kukusaidia kuanzisha biashara.
4. Fedha: Vyanzo vya fedha ni akiba kwa mjasiriamali. Kama umeajiriwa kopa kwa ajili ya biashara, pia pokea msaada kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa au rafiki. Wakati mwingine unaweza kutafuta wawekezaji kama biashara ni kubwa. Kwa msaada zaidi tembelea ‘smallbusinessfinancing.com’.
5. Maandalizi: Baada ya hatua hizo  fanya maandalizi, fanya mchanganuo kujua wateja wako ni nani, wanapenda nini, uwezo wao wa kununua. Jipange namna gani taarifa zitawafikia endapo utaanzisha biashara.
Biashara ni matangazo. Pia kama utahitaji wafanyakazi, ni muda mwafaka kuchanganua utaanza na wangapi kwa nafasi zipi. Fikiria zaidi mahitaji ya biashara unayotarajia kuanzisha kwa mfano leseni, vibali na  eneo la biashara.

6. Anzisha biashara: Baada ya mipango na maandalizi kukamalika unashauriwa kuanzisha biashara. Tangaza biashara yako, fanya  tafrija fupi, karibisha familia, jamaa na marafiki ili wajue biashara yako.
Katika tafrija hiyo unaweza kupata wateja au mtandao wa biashara yako. Unaweza kuanzia hapo.
7. Fanya marekebisho ya mipango: Wahenga walisema mipango sio matumizi kwa kuwa inawezekana  kabisa uliyoyapanga kabla ya kuanza biashara, yakawa tofauti.
Kutokana na hali hiyo chukua fursa ya kufanya marekebisho haraka iwezekanavyo na kuboresha maeneo yenye mahitaji.
+255753 686 848

Sunday, May 13, 2012

Wanaharakati Wakemea Vitisho Kwenye Mchakato Wa Katiba




TAMKO DHIDI YA VITISHO, VIKWAZO NA VITENDO VYA VIONGOZI
VINAVYOTIA WANANCHI HOFU KATIKA KUSHIRIKI MCHAKATO WA KATIBA
MPYA TANZANIA

Jukwaa la Katiba Tanzania na Baraza la Katiba Zanzibar tumeendelea
kufuatilia maandalizi ya mchakato wa kuandika Katiba mpya ikiwa ni
pamoja na kuteuliwa na kuapishwa kwa Tume ya Katiba; Hotuba mbalimbali
za viongozi wa kitaifa kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya pamoja na
mwitikio wa wananchi kwa ujumla.

Kwanza, tunawapongeza wote walioteuliwa kulitumikia taifa letu kama
wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania. Kwa maoni yetu, Tume
iliyoteuliwa imesheheni watu wenye sifa, uwezo na uweledi mkubwa kiasi
kwamba kama itazingatia misingi mikuu ya uundaji wa Katiba Mpya na ya
Kidemokrasia inaweza kufanya kazi hiyo vizuri sana. Kwa madhumuni ya
kujikumbusha, baadhi ya misingi hiyo ni ushiriki mpana wa wananchi,
usikivu na ukusanyaji maoni unaozingatia uhuru kwa kila mtanzania
kutoa maoni yake bila kukwazwa, kuzuiwa au kutishiwa. Hata hivyo
tumesikitishwa   .... Soma zaidi:

Thursday, May 10, 2012

Jk atosa DC 51, aibua 70 wapya

10th May 2012
Chapa
Maoni
  Wamo wabunge na waandishi kibao
  Watapigwa msasa na kupewa mtihani
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Rais Jakaya Kikwete ameteua wakuu wa wilaya huku akiwaacha 51 wa zamani na kuteua wapya 70.

Miongoni mwa walioteuliwa, vijana wenye umri kati ya 35 hadi 40 ni 40, wanawake 43 wakiwamo wabunge wa Viti Maalum watano, huku waandishi wa habari watano wakiteuliwa kushika wadhifa huo.

Akitangaza wakuu hao wa wilaya jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uteuzi wa vijana umezingatia pia kuwajengea uwezo kama viongozi wa baadaye.

Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Hawa Ghasia (Tamisemi), William Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge), Naibu Mawaziri, Kassim Majaliwa (Elimu) na Aggrey Mwanri (Tamisemi), Pinda alisema wakuu wa wilaya 51 walioachwa ni kwa sababu mbalimbali, ikiwamo umri, maradhi na utendaji.

Pinda alisema mchakato huo umechukua muda mrefu kwa sababu ya kuongezeka kwa wilaya mpya 19 kutoka 114 hadi 133; hivyo ilichukua muda kuwachambua na kuwapanga.

“Tumetoa wiki moja, wakuu hawa wajiandae kwenda kwenye vituo vyao vya kazi, watatakiwa kuapa mbele ya mkuu wa mkoa halafu tutawapatia mafunzo kwa wiki mbili pale Dodoma tena nimewaambia watu wa Tamisemi wawape mtihani kabisa,” alisema.

Alisema mafunzo hayo yatawahusisha pia wakuu wote wa mikoa na makatibu tawala wote.

Alisema: “Sitaki iitwe semina. Ndio maana nimesema wapewe mitihani. Tunataka wakuu wa mikoa na wilaya watekeleze majukumu yao ipasavyo.”

MATUMIZI YA  FEDHA ZA UMMA

Akizungumzia matumizi ya halmashauri, Pinda alisema serikali imetoa maelekezo kwa wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya na mikoa kupitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2010/11 na kutoa majibu ya hoja zote kabla ya Desemba, mwaka huu.

Alisema lengo ni kuhakikisha kwamba katika Mkutano wa Bunge la Februari, serikali inakuwa na majibu yote ili kuyatoa bungeni kwenye Mkutano wa Bunge wa Aprili.

“Tumetoa miezi mitatu kuanzia Mei wapitie na kujibu hoja zote za CAG kisha wazipeleke mkoani kama mkoa hautaridhika wazirudishe tena hadi tupate majibu sahihi. Tunataka itakapofika Januari serikali iwe imeshapata majibu ya uhakika,” alisema Pinda.

Pinda alisema: “Nimewaambia wenzangu wa Tamisemi tusiendelee na hii hoja ya onyo, hatutafika mbali. Anayekutwa na kosa msimamisheni na apelekwe mahakamani akapambane na sheria.”

WAKURUGENZI WAWILI MATATANI

Kutokana na msimamo huo, Pinda, alisema ametoa maagizo ya kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Sengerema na Misungwi na kisha wafikishwe mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.

Aliwataka pia madiwani kuwa makini wanapopitia hesabu za halmashauri pamoja na ripoti ya CAG ili kuongeza utendaji na uwajibikaji kuanzia ngazi ya chini.

Alisema maelekezo hayo yametolewa pia kwa wizara zote pamoja na mashirika ya umma kuhakikisha yanajibu hoja za CAG na kuziwasilisha kwenye wizara za kisekta kwa ajili ya kujiridhisha.

AMSHUSHUA KIMORO

Akizungumzia Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimoro, ambaye hivi karibuni alitangaza kujiuzulu wadhifa huo, Pinda alisema ameshangaa kusikia hivyo kwa kuwa alikuwa kwenye orodha ya wale waliokuwa wameachwa.

“Rais alisema tusitangaze bila kuwaarifu watakaoachwa. Alijua ataondolewa. Sasa tunashangaa kwa nini alienda kujitangaza…huyu angekuwa tu mkweli,” alisema Pinda na kusababisha kicheko katika mkutano huo.

Bila kufafanua kwa undani, alisema pindi inapotokea mteule wa Rais anaachwa kwenye uteuzi mwingine kama siyo kwa sababu za umri ama maradhi, hizo sababu zingine zinakuwa nzito.

Hata hivyo, Kimoro alipokuwa akitangaza kujiuzulu wadhifa huo alidai kuwa ni kwa sababu serikali imeshindwa kuwawajibisha watendaji ambao siyo waaminifu, serikali kuruhusu kampuni za kununua kahawa mbichi, biashara ya vocha za ruzuku na sababu binafsi.

WAPYA WALIOTEULIWA

Miongoni mwa wakuu wa wilaya walioteuliwa na vituo vyao vya kazi kwenye mabano ni Novatus Makunga wa ITV/Radio One –Arusha (Hai); Jacqueline Liana wa gazeti la Uhuru (Magu); Muhingo Rweyemamu wa gazeti la Jamhuri (Handeni); Selemani Mzee Selemani wa Shirika la Utangazaji la Taifa –TBC (Kwimba) na Ahmed Kipozi wa TBC (Bagamoyo).

Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum, Rosemary Kirigini (Meatu), Mboni Mgasa (Mkinga), Hanifa Selungu (Sikonge), Christine Mndeme (Hanang), Shaibu Ndemanga (Mwanga) na  Chrispin Meela (Rungwe).

Pia wamo Dk. Nasoro Hamidi (Lindi), Farida Mgomi (Masasi), Jeremba Munasa (Arumeru), Majid Mwanga (Lushoto), Mrisho Gambo ambaye alikuwa ni miongoni mwa makada wa Umoja wa Vijana wa CCM aliyekuwa amepewa karipio hivi karibuni  (Korogwe), Elias Tarimo (Kilosa), Alfred Msovella (Kiteto), Dk. Leticia Warioba (Iringa) na Dk. Michael Kadeghe (Mbozi).

Wengine ni Karen Yunus (Sengerema), Hassan Masala (Kilombero), Bituni Msangi (Nzega), Ephraem Mmbaga (Liwale), Antony Mtaka (Mvomero), Herman Kapufi (Same), Magareth Malenga (Kyela), Chande Nalicho (Tunduru), Fatuma Toufiq (Manyoni) na Seleman Liwowa (Kilindi).

Aliwataja wengine kuwa ni Josephine Matiro (Makete), Gerald Guninita (Kilolo), Senyi Ngaga (Mbinga), Mary Tesha (Ukerewe), Rodrick Mpogolo (Chato), Christopher Magala (Newala), Paza Mwamlima (Mpanda), Richard Mbeho (Biharamulo), Joshua Merumbe (Bunda), Constantine Kanyasu (Ngara), Yahya Nawanda (Iramba), Ulega Abdallah (Kilwa), Paul Mzindakaya (Busega) na Festo Kiswaga (Nanyumbu).

Wengine katika orodha hiyo ni Wilman Ndile (Mtwara), Joseph Mkirikiti (Songea), Ponsiano Nyami (Tandahimba), Elibariki Kingu (Kisarawe), Suleiman Kumchaya (Tabora), Dk. Charles Mlingwa (Siha), Manju Msambya (Ikungi), Omar Kwaangw’(Kondoa), Venance Mwamoto (Kibondo), Benson Mpesya (Kahama), Daudi Ntibenda (Karatu), Ramadhani Maneno (Kigoma), Sauda Mtondoo (Rufiji), Gulamhusein Kifu (Mbarali) na Esterina Kilasi (Wanging’ombe).

Wengine katika orodha ya wateule wapya ni Subira Mgalu (Muheza), Martha Umbula (Kongwa), Agnes Hokororo (Ruangwa), Regina Chonjo (Nachingwea), Wilson Nkhambaku (Kishapu), Amani Mwenegoha (Bukombe), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Rosemary Senyamule (Ileje), Luteni Kanali Ngemela Lubinga (Mlele), Iddi Kimanta (Nkasi) na Lucy Mayenga (Uyui).

WA ZAMAMI WALIOPONA

Katika orodha ya waliopona, Waziri Mkuu, alisema baadhi wameteuliwa na kubaki kwenye wilaya walizokuwa wanaziongoza na wengine wamehamishwa.

Aliwataja waliobaki kuwa ni James Ole Millya (Longido), Mathew Sedoyeka (Sumbawanga), Fatuma Kimario (Igunga), Kapteni mstaafu James Yamungu (Serengeti), Luteni mtaafu Abdallah Kihato (Maswa), Sarah Dumba (Njombe), Jowika Kasunga (Monduli), Elizabeth Mkwasa (Bahi) na Kanali Issa Njiku (Misenyi).

Wengine ni John Henjewele (Tarime), Elias Lali (Ngorongoro), Raymond Mushi (Ilala), Francis Miti (Ulanga), Evarista Kalalu (Mufindi), Mariam Lugaira (Misungwi), Anna Magowa (Urambo), Anatory Choya (Mbulu), Fatma Ali (Chamwino), Deodatus Kinawiro (Chunya), Ibrahim Marwa (Nyang’wale) na Dk. Norman Sigala (Mbeya).

Katika orodha hiyo aliwataja pia Moshi Chang’a (Mkalama), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Georgina Bundala (Itilima), Halima Kihemba (Kibaha), Manzie Mangochie (Geita), Abdula Lutavi (Namtumbo), Zipporah Pangani (Bukoba), Dk. Ibrahim Msengi (Moshi), Kanali Cosmas Kayombo (Kakonko), Lembris Kipuyo (Muleba), Elinasi Pallangyo (Rombo), Queen Mlozi (Singida), Juma Madaha (Ludewa), Angelina Mabula (Butihama), Hadija Nyembo (Uvinza) na Ernest Kahindi (Nyasa).

Wengine ni Peter Kiroya (Simanjiro), John Mongella (Arusha), Baraka Konisaga (Nyamagana), Husna Mwilima (Mbogwe), Sophia Mjema (Temeke), Francis Isaac (Chemba), Abihudi Saidea (Momba), Khalid Mandia (Babati) na Anarose Nyamubi (Shinyanga).

Kadhalika wamo Dani Makanga (Kasulu), Amina Masenza (Ilemela), Mercy Silla (Mkuranga), Christopher Kangoye (Mpwapwa), Luteni Edward Lenga (Kalambo), Halima Dendego (Tanga), Lephy Gembe (Dodoma), Said Amanzi (Morogro), Jackson Msome (Musoma) na Elias Goroi (Rorya).

Aliwataja Luteni Kanali Benedict Kitenga (Kyerwa), Erasto Sima (Bariadi), Nurdin Babu (Mafia), Khanifa Karamagi (Gairo), Gishuli Charles (Buhigwe), Saveli Maketta (Kaliua) na Darry Rwegasira (Karagwe).

CHANZO: NIPASHE
0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni

Saturday, May 5, 2012

4 Tips For The Successful Businessman


I have a passion for the bald eagle or Haliaeetus Leucocephalus
according to his scientific name. I have this passion as long as
I can remember. But it is not a logical passion. I am Dutch and
a passion for a bird of prey that is common in The Netherlands
would be more obvious. But life is full of inexplicable surprises
and left me with this passion for the bald eagle, the national
symbol of the United States of America. I have seen the
eagles only once in my life in their natural habitat and that
was during a holiday in British Columbia in Canada.

When I read about bald eagles and about the way they live, I
always start thinking about what a businessman can learn from
them in order to become successful and that is what this article
is about.

1. Vision

Bald eagles are birds that can often be found on very high
altitudes. There they soar and with their very sharp eyesight
they have a clear view on the world below them and especially
on the prey they want to catch; fish, that is what they like
most.They can see the milky white spot in the water from a
distance of many miles. In high places they build their nests.
On a rock, on the top of a tree but always on a spot where they
have a good view on the world that surrounds them. And from
their castle they see what is happening around them and that
gives security.

The businessman should also have a clear view on what is
happening in the market. From very far he should recognize his
potential customers and "attack" them at the right moment. At
the same time he should be aware of the dangers that surround
him, anticipate, absorb the environment and be prepared to act
immediately.

2. Knowledge

Bald eagles are confined to their territories. With the seasons
some migrate but you find bald eagles only in a specific habitat
namely forests, mountains and near sea and rivers. You won't
find them in the desert. In their habitat they know what to do,
where they can find prey and which dangers surround them. By
instinct and by learning they have knowledge about the way they
have to conduct their lives and about how they have to behave
in this habitat. They will never go beyond the limitations of this
frame work. If they do, they die.

This holds a lesson for the businessman. He should know
everything about his business and when I say everything, I mean
everything. He should know all about the products he sells from
beginning to end, every detail should be an open book to him.
He can never be surprised with questions on which he has no
answers. He should know about marketing techniques, the
position and plans of competitors etc., etc. And if he doesn't
possess this knowledge by nature, he has to learn it.

3. Enough is enough

When Bald Eagles catch prey, they will catch only one fish at a
time. It is not possible for them to catch more. But they know
precisely how to catch this one fish. Their flying skills, their
strong talons and their eyesight are extremely well developed
and fit for the job. Almost every attempt to catch a prey is
successful.

This phenomenom also holds a wise lesson for the businessman.
He has to restrict himself to a number of products he can handle
and products that matches his skills and abilities. To stay in
the animal world: if you are a cow don't try to jump fences like
a horse. People will only laugh at you. It is better to sell one
product very well than ten without a satisfying result.

4. Courage

Bald eagles mate for life and they are absolutely loyal to each
other. From high altitudes the two birds tumble down in a
dangerous free fall. Mocking the laws of gravity they unite.
Only just above the tree tops they separate and fly wing by wing
to the nest. This spectacular show requires great courage. A
businessman also needs courage to be successful. He has to make
decisions about difficult and uncertain subjects. And he also
needs to know when to stop his free fall. Having courage to make
difficult decisions is not synonymous for being reckless. A
decision that leads to disaster is not a decision, but a wild
guess.

You see....the businessman can learn a great deal from this
majestic bird that embodies not only beauty, strength and
freedom but that possesses also the essential conditions and
abilities to survive.

The beginning businessman as well, who is maybe starting his
business in great uncertainty about the future, can learn from
the bald eagle:

Flying high starts with spreading your wings!

Follow Your Dreams


skyscraper 
with the word dream on the side




I have spread my dreams beneath your feet. Tread softly because you tread on my dreams.
W.B. Yeats
Go confidently in the direction of your dreams. Live the life you have imagined.
Henry David Thoreau
Every great dream begins with a dreamer. Always remember, you have within you the strength, the patience, and the passion to reach for the stars to change the world.
Harriet Tubman
Reach high, for stars lie hidden in your soul. Dream deep, for every dream precedes the goal.
Pamela Vaull Starr
All men dream but not equally. Those who dream by night in the dusty recesses of their minds wake in the day to find that it was vanity; but the dreamers of the day are dangerous men, for they may act their dream with open eyes to make it possible.
T.E. Lawrence

Our truest life is when we are in dreams awake.
Henry David Thoreau
So often times it happens that we live our lives in chains
And we never even know we have the key.
Lyrics from Already Gone, peformed by the Eagles for their 1974 On the Border album



The end of wisdom is to dream high enough not to lose the dream in the seeking of it.
William Faulkner
I like the dreams of the future better than the history of the past.
Patrick Henry
Hold fast to dreams, for if dreams die, life is a broken winged bird that cannot fly.
Lanston Hughes
You cannot dream yourself into a character: you must hammer and forge yourself into one.
Henry D. Thoreau
The future belongs to those who believe in the beauty of their dreams.
Eleanor Roosevelt
Commitment leads to action. Action brings your dream closer.
Marcia Wieder
Dreams are the touchstones of our character.
Henry David Thoreau
The question for each man to settle is not what he would do if he had means, time, influence and educational advantages; the question is what he will do with the things he has. The moment a young man ceases to dream or to bemoan his lack of opportunities and resolutely looks his conditions in the face, and resolves to change them, he lays the corner-stone of a solid and honorable success.
Hamilton Wright Mabie
The best way to make your dreams come true is to wake up.
Paul Valery
A skillful man reads his dreams for self-knowledge, yet not the details but the quality.
Ralph Waldo Emerson
Our waking hours form the text of our lives, our dreams, the commentary.
Anonymous
Hope is the dream of the waking man.
French Proverb
To unpathed waters, undreamed shores.
William Shakepeare

Friday, May 4, 2012

Msichana aongoza mtihani kidato cha sita

  Ni wa Sekondari ya Marian Girls
  Ufaulu waongezeka mwaka huu
  Shule za serikali zafanya vizuri
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Joyce Ndalichako
Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu huku msichana Faith Assenga, wa Shule ya Sekondari Marian Girls, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, akiongoza kwa wanafunzi watano bora kitaifa.

Aidha, watahiniwa 3,404 sawa na asilimia 7.73 waliofanya mtihani huo, wamefeli kwa kupata daraja la sifuri huku wanafunzi 5,635 sawa na asilimia 12.80, wakiambulia daraja la nne ambalo pia haliwezi kuwasaidia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.

Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Joyce Ndalichako, alisema ufaulu wa mtihani huo kwa mwaka huu umeongozeka kwa asilimia ndogo huku pia idadi ya wanaofanya udanganyifu ikipungua.

Alisema watahiniwa waliofanya mtihani huo walikuwa 44,190 ambapo asilimia 5.67 ambao ni 2,499 ndio waliopata daraja la kwanza, wakati waliofaulu kwa daraja la pili ni 9,126 sawa na asilimia 20.72. Alisema waliopata daraja la tatu ni 23,375 sawa na asilimia 53.08.

Hata hivyo, Dk. Ndalichako, alisema jumla ya watahiniwa 46,499 sawa na asilimia 87.58 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne ikilinganishwa na watahiniwa 49,653 sawa na asilimia 87.24 ya waliofaulu mwaka jana.

Alisema wavulana 30,466 sawa na asilimia 87.69 wamefaulu mtihani huo wakati wasichana 16,033 sawa na asilimia 87.37 ndio waliofaulu.

Kwa mujibu wa Dk. Ndalichako, watahiniwa wa shule wamefanya vizuri zaidi kuliko wale wa kujitegemea ambapo waliofaulu ni 40,635 sawa na asilimia 92.27 wakati watahiniwa 5,864 sawa na asilimia 64.75 wa kujitegemea wamefaulu.

Kuhusu waliofeli, Dk. Ndalichako alisema wavulana 2,229 wamepata daraja sifuri ikilinganishwa na wasichana 1,175 huku wavulana 3,659 wakipata daraja la nne na wasichana 1,976 wakipata daraja hilo.

Kadhalika, sekondari za serikali zimefanya vizuri kwenye matokeo hayo ambapo shule sita za umma zenye watahiniwa 30 na zaidi zimeingia kwenye shule 10 bora kitaifa wakati za binafsi zikiwa ni nne kwenye kundi hilo.

Aidha, Dk. Ndalichako alisema ufaulu umeongezeka kwa masomo ya lugha, biashara, Historia, Jiografia, Fizikia, Hesabu na Bayolojia huku ufaulu wa masomo ya uchumi, Kemia na General Studies ukiwa umeshuka.

SHULE 10 BORA


Dk. Ndalichako alisema  Marian Girls ya mkoani Pwani imekuwa ya kwanza kwa shule 10 bora zenye watahiniwa 30 na zaidi ikifuatiwa na Feza Boys ya Dar es Salaam. Shule nyingine katika kundi hilo ikianzia ya tatu ni Kisimiri (Arusha), Kibaha (Pwani), Ilboru (Arusha), Mzumbe (Morogoro), Msalato (Dodoma), Tabora Boys (Tabora), St. Mary's Mazinde Juu (Tanga) na Seminari ya Consolata (Iringa).

Katika kundi la pili, Uru Seminari ya Kilimanjaro imeongoza shule zenye watahiniwa pungufu ya 30 ikifuatiwa na Iwawa (Iringa) na ya tatu ni Maua Seminari (Kilimanjaro).

Shule nyingine katika kundi hilo ni Harrison Uwata (Mbeya), Beroya (Ruvuma), Palloti (Singida), Lutengano (Mbeya), Makita (Ruvuma), Mwanga (Kilimanjaro) na Visitation Girls (Kilimanjaro).

"Shule 10 za mwisho kitaifa katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 na zaidi ni Pemba Islamic College ya Pemba ikifuatiwa na Zanzibar Commercial ya Unguja," alisema.

Alisema nyingine ni Kongwa (Dodoma), Uweleni (Pemba), Mazizini (Unguja), Lumumba (Unguja), Ben Bella (Dodoma), Mlima Mbeya (Mbeya), Laureate International (Unguja) na Haile Selassie (Unguja).

Katika mtiririko huo, Dk. Ndalichako alizitaja shule 10 za mwisho zenye watahiniwa pungufu ya 30 ni Mbarali Preparatory (Unguja), Philter Federal International (Unguja), High View International (Unguja), Kifai Modern (Dar), Sha (Unguja), Dar es Salaam Prime (Dar), Kandoto Sayansi (Kilimanjaro), Popatlal (Tanga), Al-Falaah Muslim (Unguja) na Kiuma (Ruvuma).

WANAFUNZI BORA KITAIFA

Akizungumzia wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kitaifa, Dk. Ndalichako alisema Necta imewapanga kulingana na ufaulu wa kombi zao 'combination' kuanzia sayansi, biashara na lugha na sayansi ya jamii.

Aliwataja waliofanya vizuri zaidi kwa masomo ya sayansi kuwa ni Faith Assenga (PCM-Marian Girls), Zawadi Mdoe (PCM-Feza Boys), Belnadino Mgimba (PCM-Minaki), Jamal Juma (PCM-Feza Boys) na Imaculate Mosha (PCM-Marian Girls).

Alisema katika kundi la sayansi, wasichana bora watano kitaifa wametoka Marian Girls wakati sekondari ya wasichana Weruweru ikitoa wasichana wanne bora kitaifa wa masomo ya biashara kati ya watano.

Wakati huo huo, Necta imefuta matokeo ya watahiniwa sita waliobainika kufanya udanganyifu na wamezuiwa kufanya mtihani wa baraza hilo kwa mwaka mmoja.

Alisema watahiniwa hao walikutwa na majibu (notisi) kwenye chumba cha mtihani na kuonya kwamba baraza hilo litaendelea kuchukua hatua kali zaidi kwa watakaobainika kufanya vitendo hivyo pamoja na maofisa watakaohusika kusaidia kufanyika kwa uhalifu huo.

Aliongeza pia kuwa baraza hilo limezuia matokeo ya watahiniwa 51 ambao hawakuwa wamelipa ada ya mtihani huku likizuia matokeo ya watahiniwa 103 ambao hawakuwa na alama za maendeleo ya kila siku.

Alisema matokeo yaliyozuiliwa yatatolewa baada ya wahusika kukamilisha kulipa ada hiyo pamoja na faini na baada ya wakuu wa shule kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kila siku ya mwanafunzi.

Baraza jipya la mawaziri: Mawaziri sita watimuliwa

  Sura mpya tatu zajitokeza
  Manaibu Waziri 2 nje, 10 wapya
Rais Jakaya Kikwete amewafukuza kazi mawaziri sita waliotuhumiwa kukiuka maadili ya utumishi na kushiriki ubadhirifu wa mali za umma.
Mawaziri hao na Wizara zao kwenye mabano ni Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Cyril Chami (Viwanda na Biashara) na Omar Nundu (Uchukuzi).
Wengine ni Dk Haji Mpanda (Afya na Ustawi wa Jamii), William Ngeleja (Nishati na Madini) na Mustapha Mkulo (Fedha).
Kwenye orodha ya waliofutwa kazi wamo Naibu Mawaziri, Dk Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii) na Athuman Mfutakamba (Uchukuzi).
Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya:
Kwa upande wa mawaziri wapya ni Dk Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), William Mgimwa (Fedha) na Profesa Sospeter Muhogo (Nishati na Madini).
Pia Manaibu Waziri wapya walioteuliwa ni Dk Seif Suleiman Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii) na George Simbachawene (Nishati na Madini).
Wengine ni January Makamba Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Dk Charles Tizeba (Uchukuzi) na Amos Makala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Manaibu Waziri wengine wapya ni Dk Binilith Mahenge (Maji), Stephen Maselle (Nishati na Madini), Angela Kairuki (Katiba na Sheria), Janet Mbene na Saada Mkuya Salum (Fedha).
Mawaziri waliobaki kwenye wizara zao:
Mabadiliko hayo hayakuwagusa baadhi ya mawaziri hivyo kuendelea kuzitumikia nafasi zao.
Mawaziri hao ni Stephen Wasira (Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Samia Suluhu (Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano), Dk Terezya Huvisa (Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira).
Wengine ni Mary Nagu (Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji na Uwezeshaji), William Lukuvu (Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Uratibu na Bunge), Samuel Sitta (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), John Magufuli (Ujenzi) na Dk Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).
Mawaziri wengine ni Sophia Simba (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Bernard Membe (Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa) na Dk David Mathayo David (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).
Wengine ni Gaudentia Kabaka (Kazi na Ajira), Makame Mbarawa (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) na Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).
Mawaziri waliobadilishwa wizara:
Rais Kikwete amewabadilisha wizara baadhi ya mawaziri, miongoni mwao na wizara walizohamishiwa kwenye mabano ni pamoja na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (Waziri asiyekuwa na wizara maalum).
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi, George Mkuchika (Ofisi ya Rais-Utawala Bora), Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani (Ofisi ya Rais-Utumishi).
Pia yumo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia ( Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa).
Wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi (Afya na Ustawi wa Jamii) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Mathias Chikawe (Katiba na Sheria).
Wengine ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni naMichezo, Emmanule Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe (Maji).
Naibu Mawaziri waliopandishwa:
Kwenye orodha hiyo wamo Naibu Waziri waliopandishwa kuwa Mawaziri kamili katika wizara zao, akiwemo Christopher Chiza, (Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk Fenella Mukangara (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Wengine waliopandishwa kwa kubadilishiwa wizara ni aliyekuwa Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe (Uchukuzi) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii).
Naibu Mawaziri waliobaki kwenye wizara zao
Mabadiliko hayo hayakuwagusa baadhi ya Naibu Mawaziri akiwemo Dk Milton Makongoro Mahanga (Kazi na Ajira) na Benedict Ole-Nangoro (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).
Wengine ni Mahadhi J Mahadhi (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Goodluck Ole-Medeye (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Ummy Mwalimu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).
Pia wamo Philipo Mulugo (Elimu na Mafunzo ya Ufunzi) na Abdalla Juma Abdulla (Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
Naibu Mawaziri waliobadilishwa wizara:
Naibu Mawaziri waliobadilishiwa wizara zao ni Adam Malima (kutoka Nishati na Madini kwenda Kilimo, Chakula na Ushirika), Pereira Silima (kutoka Fedha kwenda Mambo ya Ndani ya Nchi na Gregory Theu (kutoka Fedha kwenda Viwanda na Biashara).
JK awavutia kasi watendaji wengine:
Wakati huo huo Rais Kikwete alisema uwajibishaji wa baadhi ya mawaziri, umefanyika kutokana na dhamana za kisiasa, lakini watendaji walioshiriki katika kashfa zilizipo kwenye taarifa zilizowasilishwa bungeni, watashughulikiwa.
“Kama ni shirika la umma, basi Ofisa Mtendaji Mkuu atawajibika, nitawaondoa watendaji wakuu waliotajwa kwa maana haiwezekani mawaziri peke wabebe mzigo wote wakati wahusika wengine wapo,” alisema.
Akasema watendaji hao ni pamoja na Makatibu wakuu, wakurugenzi mpaka bodi za mashirika ya umma wote hawako salama kufuatia kutimuliwa kwa mawaziri hao.
Asikiliza sauti za wabunge:
Akitangaza uamuzi huo na mabadiliko aliyofanya kwenye Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema hatua hiyo inatokana na mjadala uliofanyika bungeni na kutolewa mapendekezo ya kuwashughulikia mawaziri kadhaa, wakiwemo aliowakuza kazi.
Ubadhirifu wa mawaziri hao ulibainika kwenye ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh na ile ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema baada ya majadiliano serikalini, ilibainika kuwa baadhi ya mawaziri hawakuhusika moja kwa moja na tuhuma zilizotolewa bungeni, hivyo kuwabadilisha wizara zao.
Ripoti zote zilisomwa wakati wa mkutano wa saba wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, kiasi cha kuibua hisia za wabunge, wakitaka serikali iwashughulikiwe mawaziri hao.
Shinikizo la kushughulikiwa mawaziri hao lilichukua sura mpya pale Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alipowasilisha hoja ya Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Zitto alikusanya saini za wabunge zaidi ya 70 wakiwemo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinazotakiwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge ili kupigwa kura hiyo.
Hata hivyo, kabla ya kuwasilishwa hoja ikiwa na na saini za wabunge, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema mchakato huo ulikuwa batili kwa vile haukikidhi kigezo cha kuwasilisha taarifa yenye saini hizo ndani ya siku 14 kabla ya kutolewa hoja husika.

Thursday, May 3, 2012

MATOKEO YA FORM SIX MWAKA 2012(NATIONAL EXAMINATION RESULTS FOR FORM SIX 2012)

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

ACSEE 2012 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES)