shuku image TIA MBEYA

Thursday, March 7, 2013

HUYU NDIE STAR WA BONGO MOVIE ALIYEFUKUZWA KWAO KUTOKANA NA KUPIGA PICHA ZA UTUPU

BAADA ya picha za Msanii Rayuu kuvunja mtandaoni, ishu hiyo sasa imechukua sura mpya baada ya kudaiwa kuwa amefukuzwa kwao na sasa amepata makazi ya muda kwa mkurungezi wake Mr Chuzi ambaye mara nyingi amekuwa akimshauri kuachana na vitendo vinavyoweza kumchafulia jina lake.

Mtandao huu
ulimtafuta Rayuu ili azungumzia ishu ndipo alipodai kuwa wazazi wake walizipata habari zake ndipo waliamua kuchukua hatua hiyo tena bila hata kumpa nafasi kujitetea na kuwaeleza mambo yalivyokuwa.

Hata hivyo inadaiwa kuwa wazazi wake awali hawakujua habari hiyo lakini kuna baadhi ya watu ambao walikuwa na kinyongo na msanii huyo ndiyo waliopeleka habari hizo pamoja na picha nyumbani kwa madai kuwa wanataka kumkomoa.


Msanii huyo alidai kuwa hakuwa na njisi kwani waliofanyan hivyo ni watu ambao mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi pamoja lakini hajui ni kwanini wamefanya hivyo ingawa hataki kujua sababu kwa sababu anaweza kuchukua hatua nyingine ambayo si nzuri
TUPE MAONI YAKO

No comments:

Post a Comment