shuku image TIA MBEYA

Wednesday, May 8, 2013

NECTA WAGOMA KUFUTA MATOKEO YA IV, WATISHIA KUJIZURU

NECTA WAGOMA KUFUTA MATOKEO YA IV, WATISHIA KUJIZURU

Prof. Rwekaza Mukandala
WAKATI Serikali ikitangaza kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminika zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Philipo Mulugo alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo iliita bila ya kupokelewa na baadaye akatuma ujumbe mfupi akisema, "Sorry I'm busy call back later", alisema Mulugo kupitia simu yake ya mkononi.

No comments:

Post a Comment